Monday, May 25, 2009

wapinga kuuzwa kwa makaburi kunduchi.

Wakazi wa Ununio,Kata ya Kunduchi jijini Dar es Salaam wameandamana kupinga kuuzwa kwa makaburi katika eneo ambalo inasemekana kuna muwekezaji amenunua eneo hilo.

Wakazi hao waliandamana huku wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali hadi kwenye Ofisi za Mtendaji wa kata hiyo ili kutaka wenyeviti wa mtaa waondolewe kwa kufanya kitendo hicho cha unyama.

Wakazi hao walidai kuwa wenyeviti wa mtaa huo kwa kushirikiana na viongozi wa Manispaa wameuza eneo hilo la makaburi ya waislamu kwa mwekezaji.

Walidai kuwa kutokana na kitendo cha kuuzwa kwa eneo ambalo ni eneo la kuzikia wafu wa kiislamu ni kitendo cha ufisadi ambacho hawawezi kukifumbia macho.

“Wanauza makaburi sasa sisi tukifa tuzikwe wapi? Na kwa nini wafanye kitendo kama hiki? Walihoji baadhi wa wakazi wa eneo hilo kwa jazba.

Mwenyekiti wa Mtaa huo Bw. Fadhila Mtoro amekiri kuuzwa kwa eneo hilo ila amesema na yeye ameshtukia tu ujenzi unataka kuanza na ndipo aliposhtuka kinyume na wakazi wanavyodai kuwa amehusika.

Amesema kwa kushirikiana na wenyeviti wengine wa maeneo hayo wanafuatilia suala hilo Manispaa ya Kindondoni ili kujua nani amehusika katika kuuza eneo hilo.

Amesema anawatahadharisha wakazi hao kuwa watafuatilia suala hilo na wawe na imani nae na kusema kwa sasa amesimamisha ujenzi usiendelee katika makaburi hayo.

3 comments:

  1. Tumeshauza migodi, tumeshauza mashirika, tushauza maliasili, tumeshauza vichwa vya upara na ngozi ya albino. Hili la kuuza makaburi halinishangazi, bado kuuza Serikali tu.

    Mdau
    Faustine
    http://drfaustine.blogspot.com/

    ReplyDelete
  2. ni kweli kaka,unayoyasema ni kweli tupu

    ReplyDelete
  3. watawauza mpaka watoto na wake zetu kwa waarabu na wairan.,yaani usije kushangaa hata ufukwe wa bahari na mito ya maji na maziwa yetu yatauzwa .kwa tama ya watu wachache.

    ReplyDelete