Wednesday, January 28, 2009

washindi shindano la malkia wa sebene wachukua zawadi zao.


Washiriki wa shindano la malkia wa Sebene Ngwasuma wakiwa wamepozi katika picha ya pamoja leo asubuhi kwenye ukumbi wa Meeda Bar mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao kutoka kwa mdhamini mkuu wa shindano hilo kampuni ya bia TBL kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro premium lager.
Shindano ambalo liliandaliwa na kampuni ya Tanvisions Ltd.
Katika shindano, hilo idadi ya washiriki ilikuwa kumi ambapo mshindi wa kwanza aliweza kukabidhiwa kiasi cha pesa taslimu shilingi za kitanzania 1600'000, mshindi wa pili alikabidhiwa kiasi cha shilingi 1100'000, mshindi wa tatu 900'000,mshindi wa nne 600'000 na mshindi wa tano 500'000 na washiriki wengine watano kila mmoja akijipatia kiasi cha shilingi 400'000.
Mashindano hayo yameshuhudia nafasi ya kwanza ikikamatwa na Vivian Stephen na hivyo kuibuka na taji la malkia wa sebene kwa mwaka huu wa 2009.
Mbali na zawadi za fedha taslimu,washindi hao pia watapata nafasi ya kusoma kozi ya urembo na nywele katika chuo cha Golden Touch,chuo ambacho kinajishughulisha na kutoa mafunzo mbali mbali ya urembo.

1 comment:

  1. its good to have mashindano kama hayo..
    i do like..

    ReplyDelete