Wednesday, March 11, 2009

Mzee Mwinyi anaswa kibao diamond.

Rais mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ally Hassan Mwinyi jana jumanne katika ukumbi wa diamond jubilee jijini dar alinaswa kibao na jamaa mmoja ambaye ni muumini wa dini hiyo ya kiislamu kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni kwa mzee Mwinyi kutetea matumizi ya kondomu kwa waumini wa dini hiyo. Jamaa huyo ambaye alikuwa anajifanya kama ni fundi mitambo, alisogelea pale alipokuwa amesimama mzee Mwinyi na kujifanya kama anataka kurekebisha kipaza sauti,ghalfa aligeuka na kumzaba kibao Mheshimiwa mzee Mwinyi katika shavu la kulia.Hata hivyo jamaa huyo alikamatwa na walinzi na kutolewa nje ya ukumbi.
Mzee Mwinyi alikuwa akitoa hotuba katika baraza hilo la maulid.

pichani juu,jamaa aliyemnasa kibao mzee ruksa akitolewa nje ya ukumbi-diamond jubilee jana.

No comments:

Post a Comment