Tuesday, April 14, 2009

Vinyago:Vivutio kwa watalii au vinatudhalilisha watu weusi?

Vinyago vya kuchonga vimekuwapo tangu zama za historia na vimechukuliwa kama utamaduni wa nchi nyingi za Bara hili la Afrika, ikiwemo Tanzania. Tanzania imejijengea sifa kubwa ya kuwa na utamaduni wa vinyango vinavyochongwa na Wamakonde kutokana na mti wa mpingo (blackwood), aina ya miti ambayo hapa duniani inapatikana katika sehemu za kusini mwa Tanzania pekee.

Vinyago hivyo ambavyo vingi huwa ni sura au umbile la mtu mweusi, vimetokea kuwa vivutio vikubwa kwa watalii na hivyo kuwa biashara kubwa inayoingizia taifa fedha za kigeni.Lakini hapa inafaa kujiuliza kidogo: Vinyago hivi hununuliwa na hao Wazungu na kuvipeleka kwao ambako hufanywa mapambo katika nyumba zao.

Kwa maoni yangu, matumizi haya ya mwisho ya vitu hivi yamekuwa yanatudhalilisha sisi watu weusi. Kuna rafiki yangu mmoja aliyewahi kuishi Denmark alinieleza kuwa watoto wanaozaliwa na kukulia katika nyumba hizo huambiwa na wazazi wao kuwa watu weusi wameumbwa kama vilivyo vinyago hivyo.

Aidha wageni wao wanaotembelea nyumba hizo zenye mapambo ya vinyago nao huambiwa hivyo hivyo.Hali hii inawafanya watu weusi daima kuwa katika kudhalilishwa mbele ya mataifa ya Wazungu yanayoendelea, kitu ambacho daima hutuendeleza kuwa wanyonge mbele yao. Matokeo ni kwamba daima wanatudharau.

Kwa maoni yangu nadhani biashara hii ingeanza kupigwa vita, Tanzania hapa na kwingineko Barani Afrika, potelea mbali kama inatuingizia kipato. Naamini kabisa ingekuwa nia wao Wazungu wasingekubali kufanyiwa kitu cha namna hii.

5 comments:

  1. Kama hali ndio hiyo(sijui kwa nchi nyingine) basi ni bora hawa wachonga vinyago wajikite zaidi kwenye uchongaji wa vitu vingine kama wanyama, milima, maporomoko ya maji, nyumba za asili n.k na hii itasaidia kutangaza vivutio tulivyonavyo hapa Tanzania kuliko kuchonga mifano ya watu.

    ReplyDelete
  2. ni kweli kabisa naungana na kassima hapo juu, hii hali kwa kweli inatudhalilisha sana sisi watu weusi kwani vinakuwa vinaonesha mambo ya kale zaidi ambapo mababu zetu aidha walikuwa wanaishi bila kuvaa nguo au wanakuwa wana yale mavazi ya zamani,ya karne hizo za kale,hivyo hata watu ambao wanakuwa wanaviona hivyo vinyago wanakuwa na picha ya moja kwa moja kuwa waafrika wana maisha na namna hii kutokana na kuwa vile vinyago jinsi vilivyo,ni vema zaidi tubadilishe mtazamo wetu waafrika ili tuweze kujikomboa zaidi na mitazamo ya namna hii.

    ReplyDelete
  3. Nimepita kukusalimia ntarudi kutoa maoni

    ReplyDelete
  4. Amani, Heshima na Upendo kwako Kaka. Bob Marley alisema "emancipate yourselves fro mental slavery, non but ourselves can free our minds." Japo sina hakika na usambazwaji wa maneno hayo, lakini sitashangaa kama ndivyo. Na pili sitashangaa kama kuna wanaoweza kupinga hilo hata wakionbeshwa ushahidi kuwa udhalilishaji huo watendeka. Lakini kupigwa vita kwa biashara hii kunaweza kutokana na mengi na mojawapo ikiwa ni suala la mazingira. Mipingo inakuwa kwa miaka na kukatwa kwa masaa na kisha kusahaulika. Ile "divide and rule" ambayo mkoloni aliipandikiza kwenye ubongo wetu ndio inayoendelea sasa. Ndio inayowafanya watu wachonge lolote hata kama ni kweli latudhalilisha. Ndiyo inayowafanya viongozi wasaini mikataba inayoua wananchi kwa kuingiza bidhaa feki na hata kuwagharimu wananchi uhitaji kwa kuwa tu wao wamepata wanachotaka. Sasa ukitaka kuona kimbembe cha makala hii, ichapishe kisha peleka makala kwa wachonga vinyago uone watakavyokugombania. Kwanini? Kwa kuwa wamefungwa akili na hitaji la pesa na hawadhani kuwa wana njia nyingine ya kuishi wakiacha kuchonga wachongavyo. Lakini pia na serikali nayo haiwawezeshi katika maisha yoyote m'badala.
    Baraka kwenu

    ReplyDelete
  5. hi!ndio maana yake...vinatudhalilisha na wazungu wanavipenda coz wanapenda kuona tukidhalilika.

    ReplyDelete