Saturday, May 16, 2009

Mali za Milioni 12 zateketezwa.

Bidhaa bandia zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 12 zimeteketezwa kwa ajili ya kukomesha uingizaji wa bidhaa hizo nchini.

Bidhaa hizo zimeteketezwa na Tume ya Ushindani [FCC] kwenye Dampo Kuu la jiji la Dar e salaam lililopo Pugu.
Mwanasheria wa Tume ya Ushindani, Laiton Mhesa amesema kuwa wao wapo kwenye jukumu la kusimamia bidhaa zinazoingizwa nchini kama zina uhalali ama la.

Ameongeza kuwa iwapo watagundua kuwa bidhaa zilizoingizwa nchini ni feki na si halali kwa matumizi ya binadamu wanachukua uamuzi wa kuziteketeza bidhaa hizo bila kujali ni za kampuni gani na zina gharama ya shilingi ngapi.

Bidhaa zilizochomwa moto ni pamoja na Katon 395 za vifaa vya umeme ambavyo vilikuwa si sahihi kwa matumizi halali,box 15 za vifaa vya simu za mkononi na radio kaseti 76.

No comments:

Post a Comment