Friday, May 15, 2009

Maximo akerwa na kelele za mashabiki.

Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania, ‘Taifa Stars’, Marcio Maximo ameonekana kuweweseka na kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wiki iliyopita.

Maximo jana aliwaambia waandishi wa jijini Dar es Salaam kuwa, anakerwa na kelele anazopigiwa mtaani na mashabiki wa soka huku wakimtuhumu kutokana na kipigo cha Kongo.

“Kila ninapopita mtaani naandamwa na mashabiki kuhusu mchezo dhidi ya Kongo, inaniuma sana jinsi watu wanavyosahau mapema kuhusu mambo yote yanayotokea Stars,” alisema Maximo.

Maximo aliwataka mashabiki kufahamu kuwa Stars ipo katika harakati za kukua na si kama wanavyofikiri vichwani mwao.

No comments:

Post a Comment