Tuesday, January 19, 2010

Mambo ya ikulu, aibu tupu!

Rais Jakaya Kikwete jana aligoma kukabidhi gari la msaada wa kubeba wagonjwa, tukio hilo lililotokea katika viwanja vya Ikulu mbele ya maofisa wa Ikulu wakati Rais Kikwete alipoonesha kusita kulikabidhi baada ya utambulisho uliomfanya agundue kuwa aliyefika kukabidhiwa gari ni wa Ngorongoro badala ya Longido.

Gari hilo lililotolewa msaada na Kampuni ya CMC Automobiles Limited, lilipaswa kupewa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Arusha, lakini kwa mshangao wake, jana alifika mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Kayange Jacob.

“Wewe ni nani... ahaa, umetokea Loliondo, ahaa hii gari si ya kwako bwana, sikupi….si yako…hii ni ya watu wa Longido si Loliondo,” wewe ni nani kakutuma?” Kayange alimueleza Rais Kikwete kuwa ametumwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Isdori Shirima. Rais Kikwete aliwageukia maofisa wa Ikulu, “Hii ni nini? Hii ni kashfa, waombeni radhi hawa mliowaalika bwana.”

“Mimi mwenyewe nilifika katika kijiji hicho nikiwa katika ziara na moja ya ahadi zangu kwao baada ya kukuta hali walionayo katika kubeba wagonjwa kijijini hapo, niliwaahidi nikipata msaada wa gari, nitawapelekea na si hawa wa Loliondo, hii ni nini, hii ni kashfa,” alirudia kusema Rais Kikwete.

Hata hivyo, juhudi za Maofisa wa Ikulu, kumfafanulia rais Kikwete aligoma na kuondoka kurudi ofisini (ndani) na kuendelea na kikao kingine kilichokuwa kikimsubiri. Kayange hakuamini macho yake alipoachwa peke yake baada ya rais kutokomea ofisini huku akilalamika what is this....bwana.

No comments:

Post a Comment