Nyaya za umeme katika mtaa wa Muheza Kariakoo Dar es Salaam zikiwa futi chache kutoka katika vichwa vya watu baada ya nguzo moja kuoza na kuelemewa na uzito, na kutishia maisha ya wakazi wa eneo hilo kutokana na nyaya hizo kutokuwa na plasitiki za usalama.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Reli nchini (TRL) wakiendelea na mgomo wao jana kudai mishahara yao. Kampuni hiyo ililazimika kuwarudishia wateja wake nauli ili watafute njia nyingine za usafiri kutokana na mgomo huo wa treni ya kwenda bara.

No comments:
Post a Comment