Japhet William (30) mkazi wa Msamvu Morogoro, ameuawa na watoto wa marehemu kaka yake ili watoto hao waweze kurithi nyumba wanayogombania iliyoko maeneo la Mafiga mkoani humo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoani Morogoro, Thobias Andengenye alitoa tarifa hizo jana ofisini kwake, na kusema kuwa mauaji hayo yalitokea juzi, majira ya saa 3 asubuhi katika maeneo ya Mafiga.
Alisema William alipata kipigo cha nguvu ikiwemo kwa kushambuliwa kwa ngumi na mawe kutoka kwa watoto hao wa marehemu kaka yake na alijeruhiwa vibaya.
Kamanda Andengenye alisema Willium alifariki dunia akiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro wakati akipatiwa matibabu baada ya kuzidiwa na kipigo hicho.
Alisema kuwa uchunguzi wa awali ulibaini kuwa nyumba hiyo ni ya wazazi wake marehemu hao wawili yeye na kaka yake, na watoto hao ilikuwa ni nyumba ya babu yao.
Andengenye aliwataja watoto waliosababisha kifo hicho ni Christina Anatory (16) na George Raymond (16) wote wakazi wa Mafiga Morogoro na kusema wote wanashikiliwa na polisi kufuatia tukio hilo.
Thursday, June 10, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment