Wednesday, November 24, 2010

watanzania wepesi wa kusamehe na kusahau

Moja ya sifa kuu waliyonayo watanzania ni wepesi wa kusamehe na kusahau.
CCM na viongozi wake wanaoujua udhaifu huo.

Mwaka 2005, katika hotuba yake ya kuzindua bunge Raisi Jakya Kiwete alisema "Katika Serikali yake mara tu Wakaguzi wa hesbu (auditor) watakapogundua wizi suala hilo litafikishwa Polisi kwa hatua zaidi badala ya kungoja vikao kukaa kupitisha maamuzi."

Mwaka 2006 ripoti ya wakaguzi wa ndani na nje ikaonyesha kuwa katika Benki Kuu zimeibiwa kiasi kikubwa cha fedha na kuwataja wahusika wakiwemo wamiliki wa Kampuni ya KAGODA na kupendekeza kuwa kwa kuwa suala hilo linahusiha masuala ya kughushi ambayo ni makosa ya jinai, wahusika wafikishwe Polisi mara moja.

Alichokifanya Raisi Jakya Kikwete ni kuunda Tume tofauti na kauli yake wakati wa uzinduzi wa Bunge la 9 Desema 2005 na baadaye kuwapatia wezi hao fursa ya kurejesha fedha walizoiba Serikalini. Mpaka leo baadhi ya wezi hao ni wajube wa Kamati Kuu ya CCM.

Tarehe 18 Novemba 2010 wakati Rais Jakya Kikwete anazindua Bunge la 10 alirudia kauli yake ya kuwataka Wizi watakaogunduliwa na wakaguzi wa mahesabu wahusika kufikishwa Polisi badala ya kungoja vikao.

kwa kuwa Sheria iko wazi kabisa katika makosa ya Jinai, kuwa kurejesha ulichoiba sio kinga ya kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria wala kupatiwa adhabu stahiki kwa mujibu wa sheria.

Na kwa kuwa wapo watu mbali mbali ambao waliwahi kurejesha walivyoiba lakini sheria ikachukua mkondo wake. Mfano hai miaka ya nyuma kidogo Mhasibu mmoja wa Wizara moja aliyewahi kujipatia mishahara miwili isivyo halali; alipogundulika ndugu zake wakaomba kurejesha kiasi alichoiba ndugu yao (Mhasibu), wakaruhusiwa na wakarejesha na kukatiwa stakabadhi ya serikali ya kuirejeshea serikali kilichokuwa kimeibiwa.

Lakini kwa kuwa kurejesha kilichoibiwa sio kinga ya mtuhumiwa kutochukuliwa hatua za kisheria, Serikali ilitumia stakabadhi za urejeshaji wa fedha hizo kama ushahidi kuthibitisha kosa mahakamani; na mtuhumiwa akapatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka 6 jela. Na kwa bahati mbaya alipoteza maisha wakati akitumikia kifungo hicho.

Nini mtazamo wako kuhusu kauli za Rais Jakaya Kikwete kuhusu wanaoiba fedha Serikali wakigundulika kufikishwa Polisi alizotoa wakati akizindua Bunge Desema 2005 na baadaye wezi walipogundulika akawataka kurejesha fedha walizoiba; na Serikali yake ikashindwa kuwachukulia hatua zaidi za kisheria baada ya ushahidi kupatikana kirahisi kama ambavyo Serikali zilizomtangulia zilivyofanya kulingana mfano uliotajwa hapo juu?

Au ndio yale yale ya Watanzania wepesi kusahau na kusamehe?

1 comment:

  1. the reason for all this is NJAA.
    When a man is hungry he has no time to think how he is lead but will do anything to get his stomach full even if it means to agree to any wrong deals.

    ReplyDelete