Saturday, January 24, 2009

migomo,maandamano vyuo vya elimu ya juu na sera mbovu ya uchangiaji wa elimu ya juu.

Imekuwa na jambo la kawaida kwa vyuo vya elimu ya juu kufungwa,wanafunzi kufukuzwa vyuoni au wanafunzi kugoma mara kwa mara,
hali hii inatokana na sera mbovu ya uchangiaji gharama za masomo ya elimu ya juu,sera ambayo haiendani na uhalisia wa maisha ya kawaida ya mtanzania wa kawaida ambaye anategemea kilimo cha jembe la mkono na mvua za msimu ili aweze kwa mfano kulima pamba ili mwisho wa mwaka awauzie walanguzi ambao watakuwa wanamlipa kwa awamu hela yake.
Ikumbukwe kwamba asilimia kubwa(zaidi ya 80%) ya wanafunzi wanaosoma vyuo vya umma vya elimu ya juu wanatoka katika familia duni ambapo wazazi wao wanategemea kilimo cha jembe la mkono. Sasa basi linapokuja suala la kuwaambia wazazi wa wanafunzi hao kuchangia elimu ya juu ambayo kama tujuavyo ni gharama kubwa,inakuwa ni kitu kigumu sana,
Kwa mfano,mzazi ambaye ni mkulima katika kijiji cha kalemela au itobo,ukimwambia atoe Tsh 1.5m au Tsh laki 8 kwa mwaka ili achangie gharama za kumsomesha mtoto wake chuo kikuu ni jambo gumu sana kwake kwani thamani ya mazao yake hayawezi kufikia kiasi hicho cha fedha.
Wito wangu mkubwa kwa serikali ya jamhuri ni kuiangalia kwa umakini mkubwa sera hii ya uchangiaji wa elimu ya juu kwani inawafanya watoto wengi wa watanzania wa kawaida washindwe kuchangia hizo gharama hivo wanajikuta wanashindwa kuendelea na masomo yao kitu ambacho kitaligharimu taifa kwani tunatengeneza taifa la vijana wasiokuwa na ujuzi wa kuweza kupambana na zama hizi za utandawazi na soko huria.No comments:

Post a Comment