Tuesday, February 3, 2009

bunduki mpya arsenal...!


Andrey Sergeyevich Arshavin,kiungo wa kimataifa wa urusi,amejiunga na washika bunduki wa jiji la london wenye makazi yao kaskazini mwa jiji hilo.
kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27,uzito wa 62kg,urefu wa sm 172 na ambaye alizaliwa May 29 1981. Saint Petersburg, Russia amejiunga na washika bunduki "the gunners" akitokea klabu ya Zenit St. Petersburg ya urusi,ambapo mwaka 2006 aliwahi kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa urusi.
kuwasili kwa kiungo huyo huenda kukaleta nafuu kubwa na matumaini mapya kwa vijana wa mzee wa kifaransa Arsene wenger ambaye kwa msimu huu timu yake imekumbwa na jinamizi la majeruhi (wakiwemo Cesc Fabrigas,Tomas Rosicky,Edwardo,Theo Walcott n.k)huenda kuliko timu nyingine yeyote katika ligi ya uingereza,na hivyo kusababisha kutofanya vizuri kwa timu yake katika ligi ya uingereza inayoendelea kwa sasa.
Reported by our reporter R.Michael,
U.K.

1 comment:

  1. Mambo vp wakuu.....

    hapa Lazima watatutambua...kuwa sisi si washika bunduki tu...bali ni wafyatua risasi pia....

    Amani kwenu

    ReplyDelete