Monday, February 23, 2009

PCB na Liyumba

Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa Nchini (Takukuru), imesema imefanya jitihada zote, lakini imeshindwa kumpata aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba, ambaye ameshitakiwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu katika kesi ya kuisababishia serikali hasara ya Sh. 221, 197,299,200.95 ya mradi wa maghorofa pacha ya benki hiyo.

Ofisa Uhusiano wa Takukuru, Doreen Kapwani, aliiambia Nipashe jana kwamba taasisi yake imetafuta, lakini bado haijaweza kumpata.

``Mpaka sasa hajapatikana na tunaendelea na jitihada za kumtafuta, tunaomba mtu yeyote mwenye taarifa za alipo atupatie, atapewa donge nono,`` alisema

kwa habari zaidi.

1 comment:

  1. Pongezi nyingi toka kwangu, asante sana kwa kuwa na blog katika lugha ya Kiswahili, ni shukurani kuu kwa wote wanaoendeleza na kukitukuza kiswahili katika tarakilishi na kwonyesha, hatubaki nyuma. Nitazidi kufuata maandishi yako...Asante sana..

    ReplyDelete