Saturday, February 28, 2009

stars na chipolopolo leo.

Timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo inapeperusha bendera ya nchi yetu katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zinazoshirikisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN).

Stars iko katika kundi la A ikiwa na wenyeji Ivory Coast, Senegal na Zambia na mechi zake zitachezwa katika jiji la Abidjan.

Stars inacheza mechi yake ya mwisho ya kundi A kwa kuivaa Zambia, Chipolopolo katika mchezo wa pili utakaofanyika mjini Baouke, Ivory Coast ambapo inatakiwa kushinda ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele katika mashindano hayo.

Mchezo huo unatazamiwa kuanza saa moja usiku kwa saa za Tanzania lakini kwa Ivory Coast itakuwa saa 10 jioni.

God bless Tanzania,God bless Taifa Stars.

No comments:

Post a Comment