Sunday, March 1, 2009

stars yatolewa.

Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), imeyaaga mashindano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani, CHAN, baada ya kutoka 1-1 na zambia katika mchezo ambao stars ilihitaji ushindi ama kupata sare lakini Segenal ifungwe angalau bao moja zaidi yake na wenyeji Ivory Coast.
Bao la stars limepatikana kupitia kwa Shadrack Nsajigwa,kwa mkwaju wa penalti ili hali bao la zambia lilipatikana kupitia mpira wa kona mnamo dakika ya nne ya muda wa nyongeza wa dakika sita.
Kwa matokea hayo,Stars imekuangana na Ivory Coast kwa kuyaaga mashindano hayo katika kundi lao.

No comments:

Post a Comment