Sunday, March 1, 2009

Uhaba mkubwa wa umeme TZ-coming soon!!

Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), limetahadharisha nchi inahitaji umeme wa dharura hivyo ni muhimu hatua zichukuliwe kununua mitambo ya Dowans haraka.

Tayari serikali imepingwa vikali na wadau mbalimbali ikiwemo Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, katika suala zima la kutaka kununua mitambo ya kampuni hiyo.

Taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk. Idrisa Rashid, iliyotolewa jijini Dar es Salaam jana ilieleza kuwa utafiti wa ukuaji wa sekta ya umeme nchini unaonyesha mahitaji ya nishati hiyo yanaongezeka kwa kasi na katika kipindi cha mwaka huu na 2013 kutakuwa na uhaba mkubwa wa umeme.

GONGA HAPA kwa habari zaidi.

No comments:

Post a Comment