Monday, March 9, 2009

HITS Tanzania kufuata nyayo za GTV !!

Zikiwa zimepita siku sio nyingi sana tangu lile kampuni kubwa la GTV(Great Television) kufungasha virago vyake kutokana na kufilisika,tayari mtandao mpya wa simu uitwao Excellentcoms au HITS nao unafungasha virago vyake tayari kwa kuondoka Tanzania baada ya mwekezaji wake kufilisika huko Marekani. Mtandao huo ambao ulikuja kwa kasi ya ajabu, ukiwa umejenga minara karibu kila kona ya nchi na ukitarajia kuanza kutoa huduma zake tangu December 2008, sasa umewapeleka likizo wafanyakazi wake na hatima yake haijulikani.

Pia inasemekana kuwa Barclays Bank nayo inachungulia kaburi wenye mafedha huko kaeni chonjo

No comments:

Post a Comment