Monday, March 9, 2009

mahubiri ya Mchungaji Mwakasege -Biafra tarehe 8/03/2009 Jumapili.

Somo toka mchungaji Mwakasege katika viwanja vya Biafra tarehe 08/03/ 2009.

kwa ufupi Somo la msingi linatoka katika kitabu cha Isaya Nabii sura ya 62 mstari wa 6 na wa 7.

Mungu aniambia Yerusalemu kwamba ameiwekea walinzi juu ya kuta zake ambao kazi yao itakuwa ni kumkumbusha Mungu usiku na mchana ili alitimize kusudi lake juu ya mji huo.ambalo kimsingi ni kuujenga mji huo uwe maarufu na simulizi duniani kote.Mistari hiyo ndiyo itakuwa msingi wa mafundisho yake kwa siku nane.

Isa.62[6] I have set watchmen upon thy walls, O Jerusalem, which shall never hold their peace day nor night: ye that make mention of the LORD, keep not silence,[7] And give him no rest, till he establish, and till he make Jerusalem a praise in the earth.soma Biblia ya kiswahili upate picha kamili

mchungaji alianza kufundika hivi;

kwanza napenda kutangaza mambo makubwa matatu maalumu.la kwanza ni kutoa ufafanuzi kuhusu wenzetu wa Zain ambao hawajaondoa hema lao hapa. msije mkajisikia vibaya kwa maana ndo kupendana ambako Tunmefundishwa. kwa hiyo msisikitike kwa hilo.ni wenzetu.

pili napenda kuwashukuru Praise power radio kwa kuwa mahubiri haya yatakuwa live kupita Praise power Radio.tatu ninapenda kuwajulisha kwamba mwaka huu tutakuwa na semona tatu hapa dar.pia katika semina ya pili nitakuwa niazimisha jubilii ya ndoa ya miaka 25 ni vilevile jubilei ya kutimiza miaka 25 ya kuhubiri-public. Introduction ya Familia yake na achievement icludinging one of his Daughters being underway to get a second pilot Licence.-rubani wa ndege ambaye anapewa lesseni ya pili karibuni.

huo ndo ulikuwa utangulizi then zikafuata shuhuda kadhaa za watu mbalimbali waliofunguliwa kwa kuandika maombi na kupeleka karatasi ziombewe au walipokea miujiza yao kupita kusikiliza katika Radio.

then akaanza kumwaga Zege.

ukisoma Isaya 62;6-7. unaona Mungu ameweka waombaji ambao ni walinzi. kwa hiyo kuna vitu viwili. waombaji ni sifa yao ya kwanza, then ni walinzi. kwa hiyo lazima wawe waombaji then wachaguliwe kuwa walinzi ambao kazi yao ni kuomba sI watakavyo wao; labda Mungu ailinde Yerusalem ingawa imeandikwa tuombee Yerusalem amani-Hapana

hawa kazi yao ni kumkumbusha Mungu kuhusu kusudi lake yeye mwenyewe alirorikusudia kulifanya dhidi ya Yerusalem Alifanye.kwa hiyo jambo la msingi ambalo alikuwa anaongelea ni kwamba unaweza ukawa unapita kwenye pito fulani, pendine kwa makosa yako ukajikuta uko kwenye majaribu mazito. unamlilia Mungu kwanini niko huku. sivyo unaweza kukuta ili makususdi ya Mungu aliyoyaweka ni lazima wewe upite hapo ulipopita, sasa suala la kulalamika na kuomba alisaidii. ni wewe kuomba kwanza kujua makudsudi ya Mungu ni nini. kwa hiyo kablwa ya kuomba inabidi tujue makusudi ya Mungu ktk jambo fulani ni nini. mathalani unaweza kuoa mke ambaye hana sifa ulizo taka lakini je wengine ulikuwa huwaoni? jambo la muhimu nikuomba Mungu akufunulie Makusudi yake kuhusu wewe kuwa na huyo Mke.\ kwani Mungu anajua mwisho tangu mwanzo.akasema ukisoma Mithali 19;21. kwmba moyoni mwa mwanadamu kuna mipango mingi lakini kususdi la Mungu ndilo litakalo simama.

kwa hiyo tukijifunza kuomba kujua Kusudi la Mungu. Ktika wito kuna vitu vitatu. kuna mipango ambayo Mungu anaiweka ili kufikia kusudi lake ambayo katika minapango yiho mwanadamu atapita either kwa majonzi au kwa furaha lakini lengo kubwa ni kulisimamisha kusudi la Mungu.unaweza ukapita katika majaruibu magumu lakini hutakiwi kukata tamaa au kujiinua kwani unaweza ukaharibu mipango ambayo Mungu ameikweka kupia wewe ili kutimiza kusudi lake lakini ukiharibu hilo ni lako. either ukakata tamaa au ukaomba Mungu akuondoe uende mbinguni. sawa utaenda mbinguni, lakini utakuwa hujatimiza kusudi la Mungu juu yako aliloliweka kwako kwa wakati wako hapa diniani.pia akajaribu kuelezea kutokea namna hii. Mungu anaweza kukupa mafunuo kuhusu watu fulani mathalani watumishi wa Mungu halafu wewe umeonyeshwa kama mlinzi wa ukuta wa Yerusalem ili ulinde kuhakikisha kusudi la Mungu linatimia badala yake ukionyeshwa udhaifu wa mtumishi fulani badala uombe ili Mungu anusuru hali hiyo ili kusudi lake litimie ,wewe ndo unaanza kumsengenya mtumishi yule na matokeo yake unachafua kanisa na kuleta migongano isiyo ya kawaida. au pia akasema wewe ni mlinzi let say wa makamu wa Rais halafu anasahau kurekebisha tai wewe unakuwa ndo wa kwanza kutoa siri zake nje.Pia akahoji Bangi ni mbaya au nzuri? jibu lilikuwa ni mbaya. na je Mungu kuna jambo Ambalo amelileta duniani baya ? kwani hata pale kwenye kitabu cha Mwanzo Mungu akaona kuwa vyote alivyoviumba kuwa ni vyema. pia kukawa hakuna jibu- kwa hiyo akapendekeza bangi ni nzuri , watu wakawa wananon'gona. akasema Mungu ameweka hadi serikali zipitishe sheria ya kukamata watu wanao tumia bangi kwa sababu watu wametumia bangi kinyume.. hawajajua kusudi la Mungu kuumba Bangi wao wameitumia kuvuta. kwa hiyo tujifunze kujua kusudi la Mungu. Maombi yanayotanguliza makusudi ya Mungu mbele bila kujali matokeo yanakuwa na matunda zaidi. kwa mfano mtu akija nimuombee kupata mchumba itabidi awe moyo mkubwa. kwani mimi sitaombea mchumba bali nitaombea kusudi la Mungu naweza kupata wachumba sita wote kwangu wqakawa out. mpaka yule mbaye Mungu amepanga atimize kusudi lake kuhusu maissha ya mtu huyo bila kujali.pia alitaka tuwe na mitazamo ya mbali mathalani tusiwe kama Habakuki soma habakuki chapter 2.yeye mtizamo wake ulikuwa hapahapa, akimlalamikia Mungu kumbe alitakiwa ajue kusudi la Mungu kama jinsi Mungu alivyo mueleza hapo chapter 2.

tusiwe kama Musa ambaye alidhani watu wa Mungu hawawezi kufika kaanani bila yeye, akajiinua kitu kilichomgharimu hata kaburi lake halikujulikana lilipo. hii ni mfano kwa wahubiri wanaojiinua kwani wanapoona Mungu anamuachia Roho mtakatifu anafanya kazi pale basi wanaona hata kama wakijiimua kumbe bado wako sawa kwani miujiza bado inatendeka . wanajaa viburi makanisani. wamuulize Musa. aliondoka na kina Joshua wakainuka. Paulo anafundisha Timotheo yuko nyuma yake. akitoka tu Timotheo anachukua nafasi. Mpango wa Mungu kuleta ndoa ilikua NI kutimiza kusudi lake. lakini Adam na Eva walipo vurunda alileta mpango wa Pili. Kristo kama Bwana na Kanisa kama mke ambao ni adam wa mwisho na Eva wa mwisho. mpango unaweza kubadilika lakini kusudi la Mungu liko palepale.plan A ime-fail ameleta Plan B. Lengo ni kutimiza kusudi lake.
hii ni sehemu tu ya mahubiri yake mchungaji Mwakasenge alipokuwa akifundisha katika viwanja hivyo.

Mungu na awabariki nyote.
Amina.

2 comments:

  1. Bwana asifiwe. kwa kweli nimefarijka sana na chakula cha roho , Mungu azidi kumtia nguvu mchungaji ili azidi kuturudisha kondoo wa Bwana zizini. na pia nilikua naomba namba ya Mwalimu nina matatizo sana sana ya familia yangu na kaka yangu amefungwa na nguvu za giza ili anisaidie kuomba.

    ReplyDelete
  2. thanks for good sms

    ReplyDelete