Friday, March 27, 2009

je wajua kuwa Mbunge hulipwa 7 million kwa mwezi Tanzania?

Mshahara na marupurupu ni milioni 7 kwa mwezi!
Bado vikao vya kamati na maslahi mengine!Kwa mwaka Mbunge hupata Shilingi milioni 84!
Na akimaliza muda wa miaka mitano hupata milioni 30 kama kifuta jasho!
Mwalimu wa shule ya Msingi hulipwa 150,000 kwa mwezi na kwa mwaka hupata 1,800,000! Hebu angalia tofauti ni shilingi 82,800,000 kwa mwaka!!!
kwa lipi hasa la msingi?ndio kusema kuwa wabunge ni productive zaidi ya wafanya kazi wengine wa serikali?
is it fair?
mi nadhani ndio maana tunakuwa na wawakilishi ambao hawana uchungu na mambo ya nchi hii,kama mishahara na marupurupu ya wabunge ingekuwa kama ya walimu wa shule za msingi au wafanya kazi wengine wowote wa kawaida serikalini,naamini ndio tungeweza kupawa wawakilishi wenye uchungu na nchi,wawakilishi wenye wito wa kujitolea kulitumikia taifa lao kama ilivyo wito kwa watu kama walimu au manesi.lakini kwa jinsi ilivyo hivi sasa,im not sure kama tutafika...

No comments:

Post a Comment