Wednesday, March 11, 2009

Mabilioni ya Jk ; Upuuzi na Ujinga mtupu!

Muda mfupi uliopita nilikuwa najadili na rafiki yangu kuhusu mabilioni ya JK aliyoyatoa kwa mikoa yote hapa nchini ili kuwawezesha Wajasiriamali.

Swali ambalo tumejiuliza na kukosa majibu ni kuwa ni namna gani Jk na serikali yake wanaweza kupima mafanikio ya takrima hii kwa Wananchi?

Kwa mawazo yangu ni kuwa hii nchi sasa inaongozwa kiujanja-ujanja na kisanii na inaonyesha jinsi ambavyo serkali hii inavyojitahidi kununua ujiko kijinga na kirahisi kiasi hicho. Nasikia Jk ana mpango wa kuongeza mabilioni mengine!

Hebu tujiulize swali hili; kama mabilioni hayo yangetumika kujenga barabara za kilometa ngapi za lami katika nchi hii ambayo ndiyo yenye miundo mbinu dhaifu kabisa katika eneo la Maziwa Makuu na Afrika Mashariki (ukiondoa DRC)? Pesa hizo zingetumika kujenga barabara kutoka Kibondo hadi Mwanza zingemsaidia mkulima wa Kibondo kuuza debe moja la mahindi kwa shilingi elfu tano badala ya shilingi elfu moja za sasa na kwake yeye hayo ni maendelo endelevu kuliko hizo biloni za miaka miwili tu!

Kwangu mimi, Mambilioni ya Jk ni ujinga mtupu na hayana msaada kwa Wananchi zaidi ya kutudanganya na kuwanunua Watanzania kwa bei rahisi.Yaani sisi WaTz tunauzwa kwa bei rahisi hivyo!

Ibrah.

No comments:

Post a Comment