Thursday, April 16, 2009

wakati JK akiuza sura, Kibaki kujenga reli mpya Nairobi na bandari Lamu...!

Kenya wamezindua mradi mkubwa wa ujenzi wa mtandao wa reli ya umeme kuunganisha nairobi na vitongoji vya karibu na uwanja wa ndege ,mradi huu unakadiriwa kukamilika mwaka 2011.

Sambamba na hilo wametumia pesa walizopata kwa kuuza hoteli yao ya kifahari ya GRAND REGENY kwa serikali ya Libya kuanzishia ujenzi wa bandari mpya ya LAMU,hii inatarajiwa kuwa kubwa kuliko ya mombasa na tayari pesa za kumalizia mradi huu zimepatikana,meli ya kwanza itatia nanga LAMU mwaka 2012.

Mradi wa bandari ya lamu unalenga soko la sudan kusini na sehemu ya kusini ya ethiopia na pia reli zitajengwa kwenda huko.

Tanzania chini ya jk wameshindwa kuendeleza bandari ya kusini ya mtwara kulenga soko kubwa la kusini na ile ya TANGA kulenda soko la uganda na kaskazini ya tanzania kupitia musoma,
pia pesa walizopata kwenye EPA au wanazodai kupata wameshindwa kuzitumia kwenye miradi inayopimika na badala yake wanadai kuzitumia kwenye mradi wa kufikirika wa mbolea ambao wala hatutaweza kuupima wanananchi wa kawaida,ingekuwa busara kama wangejengea vitu vya kuonekana kama wenzao walivyofanya.

2 comments:

  1. Unajua. Kila kiongozi hupimwa angalau kwa jambo moja kuu ambalo aliitendea jamii yake. Tazama viongozi muhimu wote katika historia - karibu wote wanapambanuliwa na jambo moja la kishujaa na kijasiri ambalo walilitenda. Mwalimu Nyerere alijaribu sana kujenga jamii yake ya kiutopia aliyoitamani lakini hakuweza. Leo hii tunamkumbuka kwa kutuwekea misingi imara ya amani na umoja - misingi ambayo kwa sasa inaporomoka kwa kasi na hakuna anayejali. Rais Mwinyi sijui anakumbukwa kwa lipi - mimi sifahamu. Mkapa naye sijui anakumbukwaje ingawa inasikitisha sana kuona kuwa mwanafunzi wa Nyerere na chaguo lake binafsi akitajwatajwa kila mara suala la ufisadi linapoibuka. JK bado anao muda na nafasi nyingi tu za kujenga historia yake. Hata kama angestaafu leo, nadhani atakumbukwa kama rais ambaye kwa mara ya kwanza alianzisha mikakati ya kupambana na wakubwa wenzake serikalini ambao ni mafisadi - jambo ambalo hata Nyerere mwenyewe hakujaribu kulifanya. Angekazania kupambana na ufisadi basi angejijengea historia ya pekee kwani ufisadi ni adui namba moja wa maendeleo yetu. Aendelee na vita hivi, asitishwe na asikate tamaa! Historia itamhukumu vizuri sana!

    ReplyDelete
  2. KUSEMA KWELI,TANZANIA NI NCHI AMBAYO MTU YEYOTE YULE ASINGETEGEMEA KUONA INAKUWA NI NCHI MASKINI KAMA ILIVYO SASA,UKILINGANISHA NA MALIASILI(HAPA NIKIMAANISHA UTAJIRI WAKE WA ASILI ILIYOJALIWA NA MWENYEZI MUNGU).TATIZO KUBWA LILILOPO TANZANIA NI UFISADI,KUTOKUWAJIBIKA KWA KILA MTU;i.e VIONGOZI NA WANANCHI WAKE.
    HIVYO TUTABAKI KUWA WATU WA MWISHO TU KIMAENDELEO DUNIANI MPAKA YESU ATAKAPO RUDI.UNLESS WE CHANGE AND GET EVERYBODY INVOLVED IN BUILDING THIS NATION NA KUPIGA VITA RUSHWA,ACCOUNTABILITY OF OUR SO CALLED LEADERS etc.TO BE HONEST,THERE'S SO MUCH TO DO IN THIS COUNTRY!!

    ReplyDelete