Tuesday, April 21, 2009

Wanawake Dodoma waingiliwa kimuijiza

Kwa mujibu wa taarifa ya habari ya TBC1, kijana mmoja mwenye umri wa miaka 19 pamoja na mama yake mzazi walikuwa wanashikiliwa na polisi mjini Dodoma kwa kosa la kijana huyo kufanya mapenzi na wake za watu pamoja na mabinti wengine kwa kutumia njia za kishirikina.

Kijana huyo ambaye ni mkazi wa kijiji fulani huko Dodoma alikamatwa jumatatu ya wiki hii kwenye nyumba ya mwanakijiji mmoja akiwa katika harakati za kufanya mapenzi na mke wa nyumba ile na wenye nyumba kumkamata kabla hajakamilisha zoezi lake. Na baada ya hapo kumpa kipigo kikali sana then kumpeleka kituo cha polisi dodoma.

Akitoa maelezo pale kituoni, kijana huyo alikiri kuwa mzoefu wa zoezi hilo na kwamba alipewa dawa ya mapenzi na mama yake mzazi iliyomwezesha kufanya mapenzi na mwanamke yeyote yule hata bila ridhaa yake huyo victim. ''Kama namtamani mwanamke au msichana halafu nikiona siwezi kumtongoza au akigoma, basi nachukua dawa mkononi naenda nyumbani kwao nikifika mlangoni naionyesha halafu mlango unafunguka, naingia ndani bila ya wao kuniona, halafu naenda kwa mwanamke ninayemtaka, namgonga namgonga,namgonga nikimaliza natoka'' mama mazazi alipoulizwa na polisi kuhusu kumpa dawa hiyo mtoto wake, alikataa katu katu. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kijana huyo amepewa jina la Gonga gonga kijijini pale.

Nimejaribu kureproduce niliyosikia TBC1 so yanaweza yasifanane kidogo na taarifa original. Mliopo karibu na eneo lilipotoke tukio hili mnaweza kutupatia picha nzuri.

Lakini ambacho nashindwa kuelewa ni;
1. Hiyo dawa yake in nguvu kiasi gani kumwezesha kufanya mapenzi kimiujiza vile na victims pamoja na jirani zake wasishituke au wasimwone? au wale victims nao wanaamini mambo hayo ya kishirikina? Je, dawa ile ingewezafanya kazi hata kwa waliookoka or swala tano na watu walio wa Mungu kwa ujumla?

2. Kwa nini dawa kama hizi hazitusaidia katika kuboresha sayansi na technolojia ili itupe maendeleo zaidi, why can't we research further kuona kama inaweza kusaidia kuleta maendeleo baadala ya maangamizo tu?

3. Je, kijana huyu kama itabidi ashitakiwe, atashitakiwa kwa kosa gani hapa? Kwa ushahidi ni upi?Haya mambo ya kishirikina huwa tunayapuuza wakati mwingine lakini ukweli ni kuwa mambo haya yapo na yanaathari kubwa sana kwa jamii yetu, likiwemo hili la kuwafanya wanawake bila ridhaa yao na mauaji albino.

No comments:

Post a Comment