Thursday, May 14, 2009

Jamaa aliyemshambulia Papa kwa risasi ataka kubadili dini.

Jamaa mmoja(pichani) ambaye ni mturuki aliyemshambulia kwa risasi na kumjeruhi vibaya sana marehemu Papa John Paul II miaka 27 iliyopita amesema kwamba anataka kubadili dini awe mkristo atakapotoka jela januari mwakani.

Katika taarifa iliyotolewa na mwanasheria wake, Mehmet Ali Agca alisema kwamba anataka kubadili dini awe mkristo na sherehe za ubatizo wake zifanyike jijini Vatican atakapotoka jela januari mwakani.

Agca alisema pia kwamba anataka atembelee kaburi la Papa John Paul II na akutane pia na Papa wa sasa hivi Papa Benedict XVI.

Mehmet Ali Agca alijaribu kumuua Papa John Paul II mwaka 1981 pale alipomrushia risasi wakati papa alipokuwa akipita kwenye mkusanyiko wa watu jijini Vatican.

Agca alifanikiwa kumpiga Papa John Paul risasi nne, mbili kati ya hizo zilitua kwenye tumbo lake na kumjeruhi vibaya utumbo wake, moja ilimjeruhi mkono wake wa kushoto na nyingine ilimjeruhi mkono wa kulia.

Walinzi wa Vatican walimwahi na kumkamata Agca kabla hajatimiza azma yake ya kumuua Papa

Kutokana na shambulio hilo Agca alitumikia kifungo cha miaka 19 jela nchini Italia pamoja na kwamba Papa John Paul II alimtembelea jela miaka miwili baada ya shambulio hilo na kumwambia amemsamehe pamoja na kwamba alimjeruhi vibaya.

Agca alirudishwa nchini Uturuki baada ya kumaliza kifungo chake nchini Italia na hivi sasa anatumikia kifungo kingine nchini Uturuki kwa mauaji ya mwandishi mmoja wa wa habari nchini humo kwenye miaka ya 1970 kabla hajakimbilia Italia na kufanya jaribio lake hilo la kumuua Papa.

Agca ambaye anatumikia kifungo chake kwenye jela ya Sincan iliyopo karibu na mji mkuu wa Uturuki, Ankara, anamaliza kifungo chake januari 18 mwakani.

kwa habari zaidi:

No comments:

Post a Comment