Thursday, May 28, 2009

mafisadi sasa kuanikwa kwenye mtandao.

Mbinu mpya imegundulika ya kuwataja mafisadi ili waweze kujulikana na sasa watakuwa wanaanikwa kwenye mitandao ya mawasiliano duniani kote.

Utekelezaji wa kuwaanika mafisadi hao wanaotuhumiwa ama kushitakiwa ulizinduliwa jana jijini Dar es Salaam.

Katika kutekeleza mradi huo tayari nchi mbili za Bara Ulaya ambazo ni Finland na Switzerland zimeshatoa mabilioni kiasi cha Euro 34,030 ili kuweza kutekeleza adhma hiyo.Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa [Takukuru] Dk. Edward Hoseah amethibitisha kutolewa kwa mabilioni hayo kwa ajili ya kufadhili mradi huo.

Fedha hizo zilitolewa na asasi ya Agenda Participation 2000 [AP2000] itakayoratibu na kusimamia mradi huo.Mtandao huo wa kisasa utatoa taarifa kwa Umma zinazohusu mashauri yanayodaiwa na yaliyothibitishwa kuhusu rushwa ili kuongeza uwajibikaji katika vita dhidi ya rushwa nchini.

Kwa mujibu wa taarifa hizo zilisema kuwa lengo kuu la mradi huo wa kuwaanika mafisadi ni kuweka kumbukumbu za watuhumiwa na wahusika wa tuhuma hizo.Pia kuongeza kiasi cha uwazi katika mashauri hayo ili raia waweze kutambua na kuwekwa wazi kuhusu ufisadi wa wahusika.

No comments:

Post a Comment