Friday, May 29, 2009

Barca wasikitika kukosa upinzani kutoka kwa Man U.

Timu ya Barcelona imeonyesha masikitiko yake makubwa baada ya kukosa kabisa upinzani ambao ulitegemewa kuwepo kutoka kwa timu pinzani yao ya Manchester United katika fainali za klabu bingwa barani ulaya iliyofanyika siku ya tarehe 27/05/2009.

Akiongea katika mahojiano na gazeti moja la hispania,kiungo mahiri wa timu hiyo Iniesta amesema kwamba yeye binafsi pamoja na timu ya barca kwa ujumla walitegemea kupata upinzani mkali kutoka kwa Manchester lakini tofauti na ilivokuwa imetegemewa na watu wengi,timu hiyo haikuonyesha uhai kabisa katika kulisakata kabumbu(gozi).

"Tulikuwa kama tunafanya mazoezi tu,hatukupata upinzani wowote ule,na ni jambo ambalo hatukuwa tunalitegemea kabisa katika fainali hizi",alisema Iniesta.

Akijibu swali kuhusu nani zaidi kati ya C.Ronaldo na Lionel Messi,Iniesta alisema"Messi ni bora kwa sasa kutokana na kwamba anao uwezo wa kumiliki mipira,anafunga,anatengeza nafasi kwa timu,anao uwezo wa kufunga kwa kupiga kutokea mbali,ana uwezo wa kuingia hadi kwenye box bila kujali anakabwa na beki wangapi na ni foward ambaye hakabiki kirahisi tofauti na Ronaldo ambaye katika mechi ile alionekana kudhibitiwa kabisa na C.Puyol".alimaliza.

Naye foward maridadi wa timu hiyo S.Eto'o alisema kuwa "huu ni mwanzo wa mambo mazuri;ni msimu ambao unaashiria mataji zaidi kwa klabu ya barcelona".

1 comment:

  1. hahaha,
    hahah,
    we iniesta wewe,ni ya kweli haya kweli? kwamba mlikuwa mnafanya mazoezi tu?

    ReplyDelete