Monday, May 25, 2009

Obama Amteua Mmarekani Mweusi Kuiongoza NASA.

Rais wa Marekani,Barack Obama amemteua mwanaanga mstaafu Mmarekani mweusi kuliongoza shirika la uchunguzi wa anga la Marekani, NASA. Uteuzi huo utalifanya NASA liongozwe kwa mara ya kwanza na mtu mweusi.
Rais Obama amemteua mwanaanga mstaafu Mmarekani mweusi Charles Bolden kuliongoza shirika la uchunguzi wa anga la Marekani, NASA.
Kama akipitishwa na bunge la senate, Bolden atakuwa Muafrika - Mmarekani wa kwanza kuliongoza NASA na atakuwa ni mwanaanga wa pili kuongoza NASA katika historia ya NASA.

Taarifa ya uteuzi wa Bolden ilitolewa na White House wakati NASA ikiahirisha kukirudisha nyumbani chombo chake cha usafiri wa anga (space shuttle) kutokana na hali mbaya ya hewa mjini Florida.

Wanaanga wa chombo hicho walikuwa wamemaliza kuifanyia matengenezo darubini iitwayo "Hubble Space Telescope" iliyopo kwenye orbit angani.

Bolden, mwanaanga mstaafu anajulikana kwa uzoefu wake na ameishasafiri mara nne katika safari za anga na alikiongoza chombo cha usafiri wa anga cha Marekani kilichoiweka Hubble kwenye orbit miaka 19 iliyopita.

Taarifa ya NASA ilisema kwamba ujuzi na uzoefu wa Bolden mwenye umri wa miaka 62 utaisaidia NASA katika harakati zake za utafiti wa anga katika karne ya 21.

"Watu sio tu kwamba wanamjua Bolden, watu wanampenda Bolden" alisema Profesa John Logsdon, wa taasisi ya anga katika chuo kikuu cha George Washington akizungumzia uteuzi huo wa Bolden kuiongoza NASA.

No comments:

Post a Comment