Tuesday, May 26, 2009

abiria afariki ndani ya dala dala.

Mtu mmoja mkazi wa jijini Dar es Salaam amekufa ndani ya daladala,
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Bw. Mark Kalunguyeye alisema kuwa tukio hilo lilitokea jana(25/05/2009) majira ya saa 2 usiku huko Kibamba.

Bwana Kalunguyeye alisema kuwa mtu huyo, jinsia ya kiume ambaye alikadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 55 na 60.
Amesema mtu huyo alifia kwenye gari aina ya Toyota Hiace lililokuwa likifanya safari zake kati ya Kibamba na Kariakoo.

Amesema kuwa mtu huyo aligundulika kuwa amekufa ndani ya daladala hilo baada ya gari kufika mwisho wa safari ambapo abiria wote walishuka na yeye akiwa amebaki kwenye siti ndani ya daladala hiyo.
Ndipo wenye daladala hiyo walipomsogelea na kumwambia kuwa amefika na kutopata majibu ku toka kwa mtu huyo.

Konda wa utingo wa gari hilo alipojaribu kumtingisha na ndipo alipogundua kuwa alikuwa amekufa.
Walijaribu kutoa taarifa kituo cha polisi kilichokuwa karibu na hapo na polisi kuja kuuchukua mwili huo na kuupeleka kuuhifadhi katika hospitali ya Mwananyamala.

Kamanda Kalunguyeye alisema kuwa chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika japo mwili wake ulikuwa umedhoofu na alikutwa akiwa na chupa ya maji ya uhai ambayo ilinekana alikuwa anakunywa.

No comments:

Post a Comment