Saturday, May 16, 2009

Simu za mkononi Kuanza Kusajiliwa mwezi wa saba.

Kuanzia mwezi wa saba mwaka huu, simu zote za mkononi zitaanza kusajiliwa ili kuepusha wizi na kulinda usalama wa raia juu ya matumizi ya simu hizo.
Mpango huo wa usajili wa simu za mkononi upo chini ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini ,TCRA.

Katika zoezi hilo, wateja wote watalazimika kusajili upya simu zao katika vituo vitakavyotengwa kwa ajili ya zoezi hilo.
Afisa Mwandamizi wa Teknolojia ya Mawasiliano nchini, Connie Fransis alisema zoezi hilo litaanza mwezi wa saba na kumalizika mwezi wa kumi na mbili mwaka huu nchini kote.

Connie aliyasema hayo katika maadhimisho ya wiki ya Teknolojia ya Mawasiliano ,ICT iliyoanza jana.
Alisema lengo la kusajili simu hizo ni kuondoa wizi wa simu za mkononi na kuepuka matumizi holela.

Alisema kuanzia mwezi wa saba wateja wote watakaonunua simu za mkononi watalazimika kusajili simu zao katika vituo au maduka watakakokuwa wamenunulia na kuongeza kuwa simu ambazo hazitasajiliwa zitafungwa.

Alisema zoezi hilo litarahisisha kwa wale ambao wataibiwa simu zao watakaotoa ripoti simu hizo zilizoibiwa zitafungwa na mtu aliyeiba atashindwa kuitumia.

Pia aliongeza kuwa hata mtu akiiba simu hiyo hata kama amebadilisha kadi ya simu hataweza kuitumia kwa kuwa itakuwa imeshafungwa.
Alisema zoezi hilo litaendeshwa kupitia kifaa maalum kinachojulikana kama Equipment Identification Register,EIR.

No comments:

Post a Comment