Sunday, May 17, 2009

deni la Tsh. 3000 lamuua.

Issa Hassan ,mwenye umri wa miaka 20,mkazi wa Makorora mkoani Tanga a.k.a (waja leo warudi leo), ameuawa kikatili kwa kuchomwa na kisu kifuani baada ya kushindwa kulipa deni la shilingi 3000 alilokuwa akidaiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishina Msaidizi wa Polisi, Simon Sirro alithibitisha kutokea kwa tukio hilo mkoani humo.

Sirro alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 12 jioni baada ya marehemu huyo kushindwa kulipa deni la 3000 alilokuwa akidaiwa na muuza chips.

Kamanda alisema marehemu huyo alichomwa kisu hicho baada ya marehemu kushindwa kulipa deni hilo ambalo alidaiwa kula chips na hivyo muuzaji huyo kuchukua uamuzi huo kinyume na sheria.

Alisema baada ya tukio hilo Issa alifariki dunia akiwa njiani akikimbizwa hospitali ya Bombo Mkoani humo kutokana na kuvuja damu nyingi sana.

Kutokana na tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoani humo linaendesha msako mkali mkoani humo kumtafuta mtuhumiwa aliyetambulika kwa jina la Achimwene kwa kuwa alikimbia baada ya kuona ameua.

Alisema kwa yeyote anayefahamu mtuhumiwa huyo amejificha katika nyumba yake anatakiwa atoe taarifa katika kituo cha polisi kinyume na hapo kwa atakayegundulika anamuhifadhi mtuhumiwa huyo atachukuliwa hatua za kisheria.



No comments:

Post a Comment