Tuesday, June 16, 2009

HITS-Tanzania CEO Resign.

Habari za uhakika zinaeleza kuwa yule aliyekuwa Mkurugenzi mtendaji wa HITS-TANZANIA Bw.Gerhard May (Pichani)ame-resign mnamo siku ya Alhamisi,Wakati huo kukiwa na uvumi kuwa ile kampuni ya Huawei Technologies iliyopewa tenda ya kujenga miundo mbinu ya Hits imesimamishwa kazi hiyo huku kukiwa kuna kila dalili ya kampuni hiyo ya simu kuchukuliwa na kampuni ya simu ya Orange ya nchini Uganda na ambayo tayari imeshachukua mtandao wa Hits wa nchini Uganda.
Chanzo cha habari kilidai kuwa kuna kila dalili ya yale yaliyotokea enzi za TRITEL kujirudia, kwani kabla ya kampuni ya TRITEL kutangaza kufilisika uongozi wa juu wa TRITEL ulihama nyumba walizokuwa wanapanga na kuhamia hotelini kabla ya kutokomea! Kwa sasa Bw.Chris Keeping Mkuu wa kitengo cha biashara cha kampuni hiyo ndiye anayekaimu nafasi yake.

No comments:

Post a Comment