Saturday, June 20, 2009

Jembe jipya la Arsenal!

Klabu ya Arsenal imekamilisha usajili wa nahodha wa Ajax Thomas Vermaelen ambaye Arsene Wenger amemsifia kuwa atang'ara sana msimu ujao na atasaidia kuimarisha ulinzi kwenye lango la Arsenal.

Thomas Vermaelen raia wa Ubelgiji amekamilisha usajili wake wa kuhamia Emirates kutoka timu ya Ajax ya Uholanzi.

Thomas ameingia mkataba wa muda mrefu na na klabu hiyo ya kaskazini mwa jiji London na anategemewa kuwa nguzo imara ya ulinzi katika lango la Arsenal msimu ujao.

Thomas mwenye umri wa miaka 23 alikuwa nahodha wa Ajax msimu uliopita na ingawa hupendelea kucheza beki ya kati pia ana uwezo mkubwa wa kucheza beki ya pembeni.

Arsene Wenger alimsifia mchezaji wake huyo mpya akisema kwamba atang'ara sana msimu ujao wa ligi ya Uingereza.
"Usajili wa Thomas ni miongoni mwa usajili mkubwa wa Arsenal, wote tumefurahi amejiunga nasi" alisema Arsene Wenger kwenye taarifa iliyotolewa na Arsenal.

"Thomas ni mchezaji mkubwa mwenye uzoezi wa kombe la mabingwa wa ulaya na kombe dogo la UEFA pia amekuwa akiitwa timu ya taifa ya Ubelgiji mara kwa mara".


Thomas anatumia mguu wa kushoto na ni fundi sana anapokuwa uwanjani huenda Arsenal Wenger akawa anampanga siku zingine acheze beki ya kushoto.

No comments:

Post a Comment