Sunday, June 21, 2009

Aunguzwa na Chai ya Moto Kwa Kukaa Karibu na Bosi Wake

Msichana wa kazi za nyumbani aliyetambulika kwa jina moja la Rose jana alijeruhiwa na bosi wake wa kike baada ya kukutwa amekaa karibu na bosi wake wa kiume mezani wakinywa chai huku wakitazamana.
Tukio hilo la aina yake lilitokea jana majira ya saa 3 asubuhi huko Kimara Suka nyumba ya tatu kutoka na anapoishi mwandishi wa habari hii.
Msichana huyo jana alijikuta yuko kwenye wakati mgumu baada ya kusikiliza ushauri wa bosi wake wa kiume kumwambia kuwa wanywe chai wote pamoja jambo ambalo alishakatazwagwa kukaa karibu na bosi wake huyo.

Msichana huyo jana alijisahau na kujikuta amekubali kunywa chai meza moja na bosi wake huyo na kukutwa na bosi wake wa kike na kuulizwa kwa nini anakunywa chai huku amekaa na baba huyo, na msichana huyo kujikuta akikosa majibu na kupatwa na kigugumizi.

Wakati anashangaa mama huyo ambaye jina tunalihifadhi ni mfanyakazi na mtumishi wa wizara nyeti ya Serikali aliichukua chai hiyo na kummwagia nayo usoni binti huyo huku akimwambia akakae mahali pengine na akatafute mahali pa kunywea chai na sio hapo karibu na mumewe.

Kelele zilisikika baada ya msichana huyo kuunguzwa na chai hiyo ya moto kwa kuugulia huku akitoka nje na kuomba ushauri kwa majirani nini afanye kutokana na kitendo hicho kilichomtokea.
Alipoulizwa ilikuwaje, binti huyo alielezea kuwa alijisahau na kukaa karibu na mume wa bosi wake wakiwa wanakunywa chai jambo ambalo mama mwenye nyumba alishamkataza.

Baadhi ya majirani walimwambia kuwa amekosea kwa kukaa karibu na mume wa mtu huku baadhi ya majirani wengine wakisema kuwa ni lazima wamchukulie hatua bosi wake kwa kitendo chake hicho cha kinyama.
Hadi habari hii inarushwa msichana huyo alionekana bado yupo kazini kwake hapo huku akijaribu kuwasiliana na ndugu zake ili kujua hatma aendelee na kazi ama la.

No comments:

Post a Comment