Tuesday, June 9, 2009

Kaduguda ajiengua Ukatibu wa Simba.


Katibu MKuu wa klabu ya Simba Mwina Kaduguda amejiengua katika kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya Katibu Mkuu wa kuajiriwa wa timu hiyo.
Kaduguda alitangaza kujitoa jana katika kuwania nafasi hiyo baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa kumpata Katibu wa kuajiriwa unaoendeshwa na Kamati ya Utendaji.
"Watapigaje kura kumpata Katibu wsa kuajiriwa?...nimejitoa, mizengwe ni mingi mno, bora nikae kando nisije nikaonekana mkorofi," alisema Kaduguda.
Kaduguda na wenzake jana walifanyiwa usaili katika hoteli ya Travertine Magomeni ili kuweza kumpata mtu mwenye sifa zinazotakiwa.
Mbali ya Kaduguda, wengine waliofanyiwa usaili ni Hamisi Tika na Hamisi Kisiwa.
Kamati ya utendaji ilipitia wasifu wa wanachama hao watatu wanaowania nafasi hiyo na kuwawekea mazengwe Tika na Kisiwa.
Tika ameelezwa kuwa si mwanachama wa Simba na Kisiwa ni mfanyakazi wa Moro United ambayo baadhi ya wamiliki wake ni viongozi wa Yanga.

No comments:

Post a Comment