Tuesday, June 9, 2009

Mwanafunzi aliyeua mwenzie UDSM Ashikiliwa na Polisi.

Mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) Masamba Musiba anashikiliwa na polisi kwa kupatikana na hatia ya kumuua mwanafunzi mwenzie.

Mwanafunzi huyo alifanya mauaji hayo katika Hosteli za wanafunzi hao zilizopo Mabibo ambapo alimuua msichana aliyetambulika kwa jina la Betha wa chuo cha Elimu Chang’ombe (DUCE).

Mauaji hayo yalitokea June 6, mwaka huu majira ya saa 6 usiku huko Mabibo katika hosteli za wanafunzi hao wa chuo kikuu jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Mark Karunguyeye amesema kuwa, wanamshiklia mwanafunzi huyo kwa kuwa amepoteza uhai na kukatisha masomo ya mwanafunzi mwenzake bila hatia.

Pia amewataka wanafunzi hao kutojihusisha na masuala ya mapenzi wanapokuwa vyuoni mana hayo ndio vyanzo vya kupatikana kwa vifo na vurugu nyingi katika hosteli hizo.

Yunusu Mgaya Makamu Mkuu UDSM amesema hosteli hizo zimekuwa zikikabiliwa na fujo za mara kwa mara na uvunjifu wa amani na wanafunzi kwenda na kinyume na maadili ya vyuo yanavyotaka.

Amesema mwanafunzi huyo anashikiliwa na polisi na uchunguzi unaendelea kufanyika wa kina kubaini zaidi chanzo cha kifo hicho na wale wote waliohusika na kifo hicho kama watapatikana.

No comments:

Post a Comment