Friday, June 19, 2009

Miss Sinza kufanyika leo.

Baada ya maandalizi ya takribani miezi miwili shindano la kumsaka mrembo wa Sinza ‘Miss Sinza 2009’ linatarajiwa kufanyika leo katika ukumbi wa Vatican City Sinza na kupambwa na burudani ya bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, mratibu wa Miss Sinza 2009, Somoe Ng’itu alisema kila kitu kimekamilika kuhusu shindano hilo na anatarajia mrembo atakayepatikana ataweza kufanya vizuri katika Miss Kinondoni.

“Leo ndiyo fainali ya Miss Sinza 2009, warembo wote wako katika hali nzuri ya kuonyeshana yupi ni bora zaidi ya wenzake, pia kutakuwapo na burudani mbalimbali kupamba onesho hilo,” alisema Somoe.
Mbali ya burudani kutoka kwa Wazee wa Ngwasuma, Miss Sinza 2009 itapambwa na burudani ya muziki kutoka kwa Costa Siboka na kundi la The Chocolate.


Miss Sinza 2009 imedhaminiwa na Global Publishers & General Enterprises, kampuni ya utoaji huduma za simu za mikononi ya Vodacom, Redd’s Premium Cold, Vuvuzela, Vanne Fashions na wengine.

No comments:

Post a Comment