Thursday, June 18, 2009

Mwili wa mtoto waopolewa kwenye shimo la choo

Mwili wa mtoto umeopolewa kutoka kwenye shimo la choo wakati wa zoezi la kutapisha choo hicho eneo la Buguruni Mnyamani jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile amesema kuwa, tukio hilo lilitokea juzi majira ya mchana huko Buguruni.
Amesema mtoto huyo aliopolewa kutoka kwenye shimo wakati wa zoezi wa kutapisha choo hicho kilichokuwa kimejaa.
Amesema shimo hilo ni la mwenye nyumba aliyefahamika kwa jina la Mohamed Issa, mwili huo ulichukuliwa na kupelekwa hospitali ya Amana kwa uchunguzi zaidi.
Hadi kufika jana jioni hakuna mtu ambaye alishikiliwa kuhusiana na tukio hilo.

Wakati huohuo kituo cha mafuta cha Bamaga kilichopo katika barabara ya Bagamoyo na Shekilango jana kilinusurika kuteketea kwa moto baada ya jenereta iliyokuwa ikisukuma mafuta kupata hitilafu na kusababisha moto mkubwa kuzuka katika kituo hicho.

Ilidaiwa kuwa moto huo ulianza majira ya asubuhi wakati gari la mafuta aina ya Benz liliposhika moto uliosababiswha na cheche zilizotoka kwenye jenereta hilo.
Inadaiwa kuwa na mmiliki na uongozi wa kituo hicho kuwa hasara iliyopatikana ni kati ya shilingi million 7 hadi 10. Katika tukio hilo hakuna mtu aliyepoteza maisha

No comments:

Post a Comment