Wednesday, June 17, 2009

Jeshi la Polisi Lakamata Majambazi 20.

Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kukamata majambazi sugu 20 yaliyokuwa yakihatarisha maisha ya watu na uporaji wa mali mbalimbali nchini.

Majambazi hao wamekamatwa katika kampeni maalum iliyofanyika kwa siku tano kwa kushirikiano kati ya Kanda Maalumu ya Dar es salaam na Pwani.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema kuwa wamefanikiwa kuwakamata majambazi 20 sugu na wameshawatia ndani.

Amesema kuwa kuna kampeni maalum inayoendelea sasa ambayo inashirikisha Polisi jamii, polisi maji na vikosi maalumu vilivyoandaliwa kwa ajili ya kampeni hiyo ili kuwakamata majambazi hao.

Amesema kati ya hao 4 waliokamatwa ni wale ambao walikuwa wanatumia ujambazi wa kutumia silaha, 2 walikutwa na vibali vya kifungo.
Wengine 10 waliokamatwa ni majambazi ambao walikuwa wanateka magari ya abiria katika sehemu mbalimbali za nchi na waliosalia ni majambazi wa kawaida.

Amesema teyari wameshawakamata na wapo mahabusu kwa ajili ya mahojiano maalum na kutaja wenzao wengine kama wapo.
Amesema wanaishukuru sana jamii kwa kuelewa kampeni hiyo kwa kutoa ushirikiano pindi wanapohisi kuna wahalifu kwa kutoa taarifa katika vituo vya polisi.

No comments:

Post a Comment