Monday, June 15, 2009

pikipiki yamuumbua.

Jamaa mmoja aliyekuwa anaendesha pikipiki maeneo ya Kimara Suka amejikuta amejijeruhi vibaya baada ya kuleta mikogo katika kuonyesha ufundi wa kuendesha pikipiki.

Dereva huyo aliyetambulika kwa jina la John (23) amepinduka na pikipiki hiyo majira ya saa 3 asubuhi leo kwenye maeneo anapoendesha shughuli zake hizo za kubeba abiria kwa usafiri huo.

Ilidaiwa kuwa kijana huyo huwa anaendesha pikipiki hizo kwa fujo na kugonga baadhi ya watu kadhaa mahali hapo kutokana na mzaha wake wa kuendesha kwa fujo.
Hata hivyo ilidaiwa kutokana na uendeshaji wake wa fujo wa usafiri huo baadhi ya abiria huwa wanamkwepa na kujikuta akikosa tenda nyingi za kubeba abiria kutokana na fujo zake hizo.

Inasemekana kuwa kama kawaida yake ya kuleta mzaha ya kuendesha pikipiki hizo leo amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya pikipiki hiyo kushindwa kuihimili na kupinduka nayo na kumjeruhi.

Kijana huyo alijeruhiwa vibaya na kufanya wenzake wamkimbize katika zahanati ya karibu kwa matibabu.

No comments:

Post a Comment