Sunday, June 14, 2009

maiti zaidi zaendelea kupatikana-Air France.

Wakati zoezi la kutafuta maiti za ajali ya Air France likiendelea, maiti nyingi zinazopatikana hivi sasa zinapatikana zikiwa hazina nguo hata moja.

Ndege ya Air France iliyodondoka kwenye bahari ya Atlantic juni 1 ikiwa na abiria 228 huenda iligawanyika vipande vipande kabla ya kuzama baharini.

Maiti 16 za abiria wa ndege hiyo zilizoopolewa kwenye bahari ya atlantic hivi karibuni zote zilikutwa hazina nguo hata moja na hivyo kuashiria kwamba huenda upepo mkali wa angani ulizinyofoa nguo za abiria wa ndege hiyo kabla maiti zao hazijaangukia baharini.

Maiti hizo zilikutwa zikiwa katika umbali tofauti tofauti wa kilomita 85 na hivyo kuwafanya wachunguzi wa masuala ya ndege kujadili uwezekano wa ndege hiyo kugawanyika vipande vipande ikiwa angani kabla ya kuangukia baharini.

Maiti nyingi zilizopatikana hazikukutwa na maji kwenye mapafu yao na hivyo kuonyesha pia kuwa vifo vya abiria wa ndege hiyo havikutokana na kuzama baharini

Wataalamu wa masuala ya ndege hawafikirii ndege hiyo ililipuka na kushika moto ikiwa angani kwani hakuna maiti iliyopatikana ikiwa na alama za kuungua.
Hadi sasa jumla ya maiti 50 kati ya 228 zimeopolewa kutoka kwenye bahari ya Atlantic.

Ndege ya Ufaransa namba AF 447 ilipoteza mawasiliano ikiwa angani wakati ilipokuwa ikisafiri kutoka Brazili kuelekea Ufaransa na iliangukia kwenye bahari ya Atlantic.

Ndege hiyo ilikuwa imebeba abiria 228 wakiwemo watoto saba, mtoto mchanga mmoja, wanawake 82 na wanaume 126.

No comments:

Post a Comment