Saturday, June 13, 2009

Viongozi wa DECI wapelekwa Mahakamani

Viongozi 5 waandamizi wa Taasisi ya Kupanda na Kuvuna Pesa a.k.a DECI wamefikishwa Mahakamani kwa makosa ya kuendesha shughuli za upatu nchini bila kibali husika.

Viongozi hao ambao wote kwa pamoja wanadaiwa kuwa ni wachungaji wa makanisa ya Pentekoste nchini walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana, majira ya saa saba na nusu wakiwa ndani ya gari aina ya Toyota Landcruiser iliyokuwa na namba za usajili T456 ASP huku nyuma kukiwa na gari ya polisi aina ya Defender.

Watuhumiwa hao wamefikishwa Mahakamni kujibu mashitaka mawili likiwemo la kuendesha mradi wa upatu kinyume na sheria za taasisi za fedha nchini na kuendesha mradi huo bila kuwa kibali.
Wakisomewa mashitaka hayo na Mwendesha Mashitaka wa serikali Prosper Mwangamila mbele ya Hakimu Mkazi Adi Lyamuya alidai kuwa, washitakiwa hao kati ya mwaka 2007 hadi kufikia Machi 2009 walikuwa wanachukua amana za watu bila ya kibali.

Alidai washitakiwa hao waliomba kibali cha kuendesha shughuli za kifedha lakini si cha kuchukua amana kutoka kwa wananchi.
Hivyo upande wa Mashitaka ulidai kuwa upelelezi wa haujakamilika na kuzuia kibali na kupinga kupewa dhamana kwa washitakiwa hao.

Hata hivyo,upande wa utetezi uliomba washitakiwa wapewe dhamana kwa kuwa washitakiwa wote kwa pamoja ni wachungaji wa makanisa ya Pentekoste nchini hivyo wangeweza kuathiri ibada kwa wananchi walio wengi maana wao ndio tegemeo kwa kuongoza ibada kwenye makanisa hayo.

Hakimu alipinga maombi hayo na washitakiwa wote kwa pamoja walirudishwa rumande kwa kukosa dhamana na watarudishwa tena June 17, mwaka huu kwa kutajwa tena mahakamani hapo.

Inadaiwa zaidi ya watanzania laki saba kote nchini walijiunga na taasisi hiyo na walikuwa wakipanda na kuvuna pesa na kukadiriwa kuwa na matawi zaidi ya 40 kote nchini ya taasisi hiyo.

Kutokana na kuzuiliwa kwa kuendelea na mradi huo wa kupanda na kuvuna pesa watanzania wameathirika kwa kiasi kikubwa mana wengi wao mradi huo ndio ulikuwa mkombozi wao kwa kuinua kipato kwa watu wa hali ya chini.

Wanachama wa taasisi hiyo jana walionekana kuwea na huzuni kubwa wengi wao wakiibua vilio mahakamani hapo kwa viongozi hao kupandishwa kizimbani mana hadi kufikia leo hatma ya fedha walizopanda katika tasisi hiyo bado halijapatiwa ufumbuzi.


“Tunaomba Serikali waliangalie suala hili kewa kina, kama wameshaonekana kuwa wana makosa basi watuangalie na sisi tulioweka fedha zetu tunaomba Pinda atoe tamko mana alisema tutarudishiwa tunaona kimnya wachukue hatua turudishiwe fedha zetu jamani” walilalama wanachama hao.

No comments:

Post a Comment