Thursday, July 23, 2009

Mwanamke mahakamani kwa kutishia kumuuza albino

Mwanamke mmoja amefikishwa katika Mahakama ya mwanzo ya Magomeni jijini Dar es Salaam, kwa tuhuma za kumtishia kumuuza na baadaye kumuua, Yusta Mlunge mkazi wa Kigogo Magengeni ambaye ana ulemavu wa ngozi (Albino).
Akisoma hati ya shtaka hilo , mbele ya Hakimu Mwanaidi Madeni, karani Irimina Iligi alidai mnamo April 15, saa 5:00 asubuhi maeneo ya Kigogo Magengeni mshatakiwa Rukia Hassan (43), alitenda kosa hilo.
Mtuhumiwa alikana shtaka hilo, na yuko ndani kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo kesi hiyo iliahirishwa hadi Agosti 6.
Wakati huo huo mkazi wa Tandale Muharitani Juma Mohamed (47) alifikishwa katika mahakamani hiyo, akikabiliwa na shtaka la kutoa lugha ya matusi.
Akisoma hati ya shtaka hilo, karani Irimina Iligi alidai kuwa mnamo Julai 19 mwaka huu, saa 8:00 mchana maeneo ya Tandale Muharitani, mtuhumiwa alimtukana Yahya Ngoma (69) nyumbani kwake.
Mtuhumiwa alikana shtaka hilo, na yupo rumande hadi hapo itakapo tajwa tena Agosti 8

1 comment: