Monday, July 13, 2009

Ripoti ya Mabomu Mbagala Yakamilika

Mkuu wa Mkoa wa Dar es SaLaam, Willium Lukuvi ametoa ripoti maalumu ya milipuko ya mabomu katika kambi ya jeshi Mbagala yaliyotokea na kuharibu nyumba zilizokuwepo karibu na maeneo hayo.
Ripoti hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Dar es SaLaam, Willium Lukuvi na ilifanyiwa uhakiki na kamati maalumu ambayo iliundwa kuhakiki nyumba zilizoharibika ili waweze kupatiwa fidia.
Lukuvi amesema kuwa katika ripoti hiyo nyumba ambazo ziliteketea kabisa na hakuna kitu kilichookolewa ndani zilikuwa jumla ya nyumba 235.
Nyumba 54 ziliharibika ambazo hazifai kwa matumizi ya binadamu ambazo hazikuteketea kabisa na kuanguka.
Amaesema nyumba zingine ziliathiriwa kidogo kidogo na si kuanguka chini na kufaa kwa matumzi ya binadamu.
Amesema jumla ya nyumba zote ambazo ziliathirika hata kama hazikuanguka zilikuwa jumla ya nyumba 9200.
Amesema ripoti ya awali ilionyesha jumla ya nyumba zilizoathiriwa na mabomu hayo zilikuwa nyumba 9254 ambazo si sahihi.

Amesema serikali imeshaanza mchakato wa kuwalipa fidia wananchi hao ili waweze kupata makazi.

No comments:

Post a Comment