Thursday, August 13, 2009

Ajali yatokea.

Zaidi ya watu 60 wamenusurika kifo baada ya basi walilokuwa wakisafiria liitwalo SAIBABA kuacha njia na kupinduka huko Mombo mkoani Tanga
Ajali hiyo ilitokea jana Maeneo ya Mombo ambapo basi hilo liliacha njia na kuingia porini kwa kukwepa ajali ya uso kwa uso na lori lililokuwa likija mbele yake.Basi la Saibaba lililokuwa na namba T.358 AEQ lililokuwa linatokea Mkoani Arusha kuelekea Dar es Slaam na kunusurika na ajali hiyo eneo hilo.Ilidaiwa kuwa basi lilikuwa linajaribu kukwepa ajali ambayo lori lilikuwa linakuja mbele yake na kukataa kulipisha basi hilo ambapo nyuma ya lori hilo kulikuwa na gari nyingine ilikuwa inajaribu kuovateki lori hilo na basi hilo kukwepa ajali hiyo na kuingia porini.

No comments:

Post a Comment