Saturday, October 17, 2009

Mtanzania kuandika historia mwezini

A.Thakkar anatarajia kuwa Mtanzania wa kwanza kwenda mwezini wakati atakapofanya safari hiyo mwakani.
Mtanzania huyo, ambaye ni chotara wa Kiingereza alienda Ikulu jijini Dar es salaam jana kumueleza Rais Jakaya KIkwete kuhusu safari yake na kumuaga.
Thakkar, ambaye mama yake ni mzaliwa wa Mwanza na baba Uingereza, alimwambia rais kuwa anajisikia vizuri kuwa mwakilishi wa Afrika, na hasa Tanzania kwenye safari hiyo ya angani.


"Najisikia vizuri kuwa mwakilishi wa Afrika hasa Tanzania ambako mama yangu alizaliwa, na hii itakuwa nafasi muhimu kwetu kujitangaza duniani kote na kuieleza dunia kuwa Afrika tunaweza na tuna maliasili za pekee,"alisema Takkar alipokuwa akizungumza na Rais Kikwete.

Rais alimweleza Mtanzania huyo anatakiwa apige picha nyingi atakapokwenda mwezini kwa ajili ya kujitangaza zaidi na kuinadi sekta ya utalii kwa juhudi zake zote.
Rais Kikwete alimkabidhi mwanaanga huyo bendera ya Tanzania na kusema watu wenye damu ya Tanzania wapo wengi duniani kote, lakini hawajitokezi kuitangaza nchi kama anavyofanya Thakkar.


"Ni nafasi nzuri kujitangaza kwa kuwa hauwezi kufanikiwa katika utalii bila kujitangaza na tunataraji kupitia Thakkar tutatangaza vyema utalii wetu popote atakapokuwa mwanaanga huyu angani na ardhini,alisema Rais Kikwete.

No comments:

Post a Comment