Wednesday, December 2, 2009

Lionel Messi Ndiye Mchezaji Bora UlayaNyota wa timu ya taifa ya Argentina na timu ya Barcelona ya Hispania, Lionel Messi amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa ulaya wa mwaka 2009.


Lionel Messi ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa ulaya wa mwaka 2009 au maarufu kama "Ballon d'Or" baada ya kuisaidia Barcelona kunyakua makombe matatu msimu uliopita.


Messi alitoa mchango mkubwa kwa wababe hao wa Catalan kunyakua kombe la mabingwa wa ulaya, kombe la ligi ya Hispania na kombe la Copa del Rey.


Messi alimwacha kwa mbali mshindi wa mwaka jana Cristiano Ronaldo,aliyeshika nafasi ya pili katika kura za tuzo hiyo.Messi amekuwa mchezaji wa sita wa Barcelona kushinda tuzo ya mchezaji bora wa ulaya.

No comments:

Post a Comment