Monday, December 14, 2009

Zanzibar ni giza tupu.

Zanzibar inakabiliwa na ukosefu wa umeme tokea mwanzoni mwa wiki hii na kupelekea mji huo kuwa na giza.

Tatizo hilo limetokana na kudaiwa kuwa kuna nyaya moja ya umeme inayotoka Tanzania Bara inayopeleka umeme visiwani humo kuleta hitilafu .

Umeme ulikatika visiwani humo tokea Jumanne ya wiki hii na hadi kufikia leo tatizo hilo bado halijapatiwa ufumbuzi na kudaiwa kuwa matengenezo yanaendelea.Wakuu wanaoshughulikia tatizo hilo walidai kuwa tatizo hilo linashughulikiwa na na linaweza likachukua wiki tatu mbele kutatua tatizo hilo kubwa visiwani humo.

Mmoja wa wakazi wa visiwani humo aishie maeneo ya Mpendae visiwani humo amesema kuwa wakazi wa visiwani humo wanakabiliwa na tatizo hilo zito na kufanya shughuli mbalimbali kukwama na kurudisha maendeleo ya wakazi wa Zanzibar nyuma.

“ Yaani toka Jumanne ya wiki hii hakuna umeme mji mzima ni kiza,na tatizo hili halijulikani litaisha lini” alisema.

No comments:

Post a Comment