Monday, February 15, 2010

Mr Gay World Pageant-taji la urembo la mashoga!


Mwanaume toka Afrika Kusini amefanikiwa kutwaa taji la mashindano ya urembo wa mashoga wa dunia 'Mr Gay World Pageant' yaliyofanyika jana jumapili mjini Oslo nchini Norway.Charl Van den Berg, 28, shoga toka Afrika Kusini aliwashinda mashoga wenzake toka Australia, Hong Kong, China na Hispania na kutwaa taji la dunia la kumsaka mwanaume shoga mrembo kuliko wote duniani kwa mwaka 2010.
Charl ambaye anaendesha mgahawa wa chakula mjini Cape Town nchini Afrika Kusini alitwaa taji hilo baada ya mashindano ya siku nne ya kuvaa mavazi mbalimbali yakiwemo mavazi ya kuogelea.
Taarifa kutoka kwa waandaaji wa mashindano hayo zilisema kuwa lengo kubwa la mashindano haya ni kumtafuta mtu atakayekuwa kiongozi wao katika kutetea haki za mashoga duniani.
Raia wa Australia Byron Adu, 25, alishika nafasi ya pili akifuatiwa na Rick Dean Twombley, 33, mcheza dansi toka Hong Kong aliyeshika nafasi ya tatu.
Xiaodai Muyi, 26, shoga toka China alishiriki na kushika nafasi ya nne katika mashindano hayo pamoja na hatua za China kumzuia asishiriki mashindano hayo.
Mhispania Sergio Lara, 26, akishika nafasi ya tano.

No comments:

Post a Comment