Tuesday, May 4, 2010

ninapoitafakari hotuba ya mheshimiwa rais kikwete

Ni vitisho, ni vitisho, ni vitisho tuuuuuuuuuu na ubabe wa mwenye mamlaka!

Kwanza ametoa amri rasmi kwa polisi washughulike na watakaogoma, lakini sielewi hata hawa polisi wanaoamrishwa kukamata wenzao wao wanaridhika na mshahara wao ama wao sio sehemu ya wafanyakazi wanaoishi kwa shida!!
Lakini nadhani wataenda tu ili kuitii mamlaka.

Hata wakati wa utawala wa wakoloni ambao walikuwa ni wakatili bado kuna watu ambao ama kwa kutoelewa ama kwa sababu ya njaa zao walikuwa wanajilazimisha kumshangilia bwana mkubwa wakati alipokuwa akihutubia.

Idi Amin,Sadaam Hussein walikuwa wakishangiliwa sana wakati wa hotuba;Idi Amin (hasa na waingereza waliokuwa wakiishi uganda kwa wakati huo), sababu kuna watu wamepangwa kiprotokali ili washangilie japo si kwa hiari zao na kamera zinawekwa makusudi ili kuonyesha kuwa mheshimiwa anaungwa mkono!

Hawa wooote waliokuwepo hapo ni watu ambao wana dhiki na shida na wasiojiweza lakini kwa vile wana ule mtazamo wa ''zidumu fkra sahihi za mwenyekiti wa CCM" vichwani wao, hata hawajui kuwa tuko katika mfumo mwingine zaidi ya kuwa atamkalo kiongozi wa nchi ndilo sahihi ukizingatia kuwa ndiye yule yule mwenyekiti wa chama anayedhaniwa kuwa yuko sahihi wakati wote (aliyeteuliwa na Mungu).

Inasikitisha sana pale nguvu na vitisho vinapotumika kuzima harakati za kudai haki za wafanyakazi na jamii kwa ujumla na haitatokea kamwe serikali iruhusu maandamano au mgomo, lazima itakuja na excuses nyingi kama hizi na kuponda kusiko na mantiki!

Kuna sababu ya msingi ya serikali kushindwa kuboresha maslahi ya watumishi na wananchi wake kwa ujumla?
Kwanini bwana mkubwa (mwajiriwa namba 1) anafiKiria kukopa tu kwa ajili ya kila jambo hadi hata mishahara?
Hivi tu maskini wa raslimali kiasi hicho kwamba hazitoshi kutuondoa hapa tulipo mpaka tukakope sehemu halafu tuanze kurejesha kwa riba kubwa, ama tu maskini wa akili kwamba hatufikirii jinsi mbadala ya matumizi ya tulivyo navyo?

Kwa hiyo sisi ili tuneemeke ni hadi tukooooope mpaka basi!
Umoja ni nguvu, na hata kama wengi hawa wana uwezo mdogo wa kutafakari na kutafakuri, bado wana nguvu nyingi kwa kutoelewa kwao na ndio hao wanaonekana kushangilia kila jambo linalotoka kwa mheshimiwa!

Lakini hii nguvu ya mwisho inajaribu kutumika na kutoka kwa kiongozi wa nchi, sababu kuna huu mkutano wa uchumi duniani unafanyika hapa na hali hii huenda ikatia shaka kidogo katika nchi hii ambayo imekuwa ikifikirika kuwa ni kisiwa cha amani simply because haturushiani risasi kama majirani zetu.

lakini ukweli unabaki pale pale pale kwamba serikali haihitajiki kutoa vitisho kwa wananchi wake bali kutatua matatizo yao yanayowakwaza kila siku, serikali haihitaji kujenga uadui baina yake na wananchi inayowaongoza bali urafiki na kwa jinsi hii itasaidia kupambana na rushwa, ufisadi na hatimaye kujenga nchi yetu ya Tanzania!

No comments:

Post a Comment