Saturday, May 7, 2016

sakata la uhaba wa sukari nchini

Mfanyabiashara mmoja amekamatwa na tani 4,900 za sukari Mbagala, Dar es salaam na kikosi kazi kilichoundwa kufanya upekuzi. 
Inasadikiwa kuwa wafanyabiashara wa bidhaa hiyo wamekuwa sio waaminifu na kuficha bidhaa hiyo muhimu kwa jamii baada ya serikali kutoa maelekezo kwa wafanyabiashara hao kuwa wanapaswa kuuza bidhaa hiyo kwa bei elekezi ya shilingi 1800 kwa kilo.

Pekua pekua hiyo imeanza mara baada ya rais kutoa Dkt John Magufuli kutoa tamko la kufanya msako nchi nzima kubaini wafanyabiashara wasio waaminifu walioficha bidhaa hiyo katika kuonyesha kupinga kwao kuuza bidhaa kwa kutumia bei elekezi iliyotolewa na serikali. 
Wafanyabiashara watakaobainika kutenda kosa hilo watakabiliwa na aidha faini kali,kushitakiwa mahakamani ama kufutiwa leseni zao za biashara.



No comments:

Post a Comment