Zaidi ya visima 80 vilivyoharibika katika halmashauri ya manispaa za Ilala, Kinondoni na Temeke jijini dsm vitakarabatiwa ili viweze kutoa huduma ya maji kwa wakazi wa wilaya hizo.
Hayo yamesemwa na msimamizi wa mradi wa kufufua huduma za visima jijini dar bwana Aziz Ally.
Bwana Aziz alisema kuwa uchunguzi uliofanyika hivi karibuni umeonyesha kuwa visima vingi katika manispaa hizo vimeharibika vibaya na vinahitaji matengezeno ya haraka.
Aidha bwana Aziz amebainisha kuwa tayari ofisi yake imeshawasilisha kwenye mamlaka husika orodha ya visima vinavyotakiwa kufanyiwa ukarabati pamoja na mchanganuo wa gharama za kazi hiyo.
"Tayari tumekamilisha utafiti wa kufufua visima vilivyokufa kwa katika manispaa zote tatu za jiji la dar" alisema bwana Aziz.
Bwana Aziz alisema endapo ukarabati utakamilika basi itasaidia kupunguza tatizo la maji kwa wakazi wa jiji la dar kwa 75%.
Alisema pamoja na kubaini visima vilivyoharibika, pia kuna baadhi ya vitongoji ambavyo havina visima vya maji kabisa .
"Mimi nashirikiana na wenyekiti wa vitongoji tunatafuta maeneo ili tuweze kuchimba visima vipya na wakazi wa maeneo hayo waweze kunufaika na visima hivyo" alisema.
Friday, May 28, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment